Naibu Waziri wa Nishati Mh. Judith Kapinga amelieleza bunge, jijini Dodoma kuwa gharama za mradi wa kujenga kituo cha kupooza umeme kitakachojengwa Dumila kitagharimu dola za Marekani milioni 39.
Maelezo hayo ameyatoa alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Kilosa, Mh. Palamagamba Kabudi aliyeuliza ni lini Serikali itajenga sub-station ya umeme katika eneo la Dumila-Kilosa.
Naibu waziri Kapinga ameliambia bunge kuwa, Serikali kupitia shirika la umeme Tanesco itautekeleza ujenzi wa mradi huo wa njia ya kusafirishia umeme wa msongo wa kilovoti 220 kutoka Morogoro hadi Dumila yenye urefu wa kilomita 66 na ujenzi wa kituo cha kupooza umeme eneo la Magole-Dumila kupitia mpango wa gridi imara awamu ya pili unaotarajia kuanza mara tu baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza mwaka 2026.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kapinga ameliambia bunge kuwa, kazi zinazofanyika katika hatua za awali za mradi huu ni kufanya upembuzi yakinifu na taratibu za kutafuta fedha za kwa ajili ya kutekeleza mradi huu.
Aidha, Naibu Waziri ameeleza kuwa, kukamilika kwa mradi huo kuwezesha eneo la Dumila na maeneo jirani kuwa na umeme wa uhakika.