Katika utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, serikali imesema zaidi ya bilioni 80 zimetumika kusambaza umeme kwenye vijiji mbalimbali mkoani Singida.
Akizungumza na wananchi, Naibu waziri wa Nishati, Mh. Judith Kapinga ameeleza kuwa lengo la Serikali ya awamu ya Sita ni kuhakikidha inasambaza umeme kwenye vijiji na Vitongoji vyote.
Naibu Waziri Kapinga amesema kwa mwaka huu wa fedha wa 2024/2025 serikali imekusudia kufikia zaidi ya vitongoji 4000. Akiangazia msukumo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuongeza kasi ya usambazaji wa umeme nchini, Naibu Waziri Judith Kapinga ametaja ubinifu na uchapakazi wa Mh. Rais.
Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Mh. Ramadhan Abeid Ighondo amepongeza Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ufanisi mkubwa katika utekelezaji wa miradi ya kuwainua wananchi wa Tanzania.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Singida Kaskazini, Mh. Godwin Gondwe ameahidi kuongeza ufuatiliaji kwa ukaribu wa ukamilishaji wa miradi yote wilayani kwake.