728 x 90

Serikali ya Rais Samia yaongeza kasi ununuzi wa vifaa tiba.

  • June 25, 2024
Serikali ya Rais Samia yaongeza kasi ununuzi wa vifaa tiba.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na vifaa tiba kwenye zahati, vituo vya afya na halmashauri mbalimbali nchini.

Hayo yameelezwa leo bungeni jijini Dodoma, na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mh. Zainab Katimba wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum, Mh. Maryam Azan Mwinyi aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itaweka vifaa tiba katika majengo ya huduma za mama na mtoto katila halmshauri mbalimbali nchini.

Mh. Katimba amesema katika kipindi cha mwaka 2022/23 hadi 2023/24, jumla ya shilingi bilioni 186.3 zimetumika kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba vikiwemo vifaa vya huduma ya mama na mtoto.

Naibu Waziri Katimba amesema Serikali ya awamu ya Sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mwaka wa fedha 2024/25, Serikali imetenga shilingi bilioni 66.7 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba ambapo kipaumbele kimewekwa kwenye vifaa tiba vya huduma za mama na mtoto kwenye vituo vyenye upungufu kote nchini.