Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewajumuisha kwenye mpango wa taifa, watu wanaotambulika kuwa kwenye makundi maalum juu ya upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa kwa makundi hayo.
Utaratibu wa kusajili na kuwatambua watu waliopo katika makundi ikiwemo wafungwa na mahabusu ni kupitia maombi maalum kutoka kwa wakuu wa Gereza katika wilaya husika.
Utaratibu wa usajili wa makundi hayo unafanywa na NIDA kwa kushirikiana na Wakuu wa Magereza na Maafisa wa usajili wa wilaya husika.
Serikali inatambua kuwa baadhi ya wafungwa na mahabusu wamekwisha kusajiliwa walipokuwa uraiani kabla ya vifungo vyao. Serikali ya awamu ya Sita kupitia NIDA inaendelea kuwa utayari wa kufanya usajili na utambuzi kwa watu wote waliokidhi vigezo ikiwemo wafungwa na mahabusu kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza.
Msimamo huo wa Serikali umesemwa bungeni kupitia Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Daniel Baran Sillo, wakati akijibu swali la Mh. Asia Halamga, mbunge wa viti maalumu, aliyetaka kufuhamu Serikali in mpango gani wa kuwapa vitambulisho vya Taifa wafungwa pamoja na mahabusu.