728 x 90

Jitihada za Rais Samia Suluhu kuboresha ustawi wa jamii wa watu wa makundi maalumu.

  • July 7, 2024
Jitihada za Rais Samia Suluhu kuboresha ustawi wa jamii wa watu wa makundi maalumu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametajwa kama kinara wa mabadiliko chanya kwa jamii ya watu wanaohesabika kuwa katika makundi maalum.

Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan amepongezwa kwa kuimarisha huduma za ustawi wa jamii kwa makundi maalumu. Hadi kufikia mwezi Machi, 2024, Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan ilikuwa imefanikiwa kuwatambuajumla ya watu wenye ulemavu 11,434 ambapo kati ya hao wanawake ni 6,131 na wanaume ni 5,303.

Kwa maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, watu wote hao wameunganishwa na huduma mbalimbali, ikiwemo kuwapatia mafuta maalum kwa watu wenye ualbino 2,960 kulingana na uhitaji wao.

Mbali na hao, Serikali ya awamu ya Sita imewatambua na kuwaandikisha jumla ya wazee 574,321 katika mikoa 26, wakiwemo wanawake 359,582 na wanaume 214,739. Kati ya wazee wote hao, tayari Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imesahwapitia wazee wanawake 219,455 na wazee wanaume 145,829 vitambulisho vya wazee kwa ajili ya msamaha wa matibabu.

Katika muendelezo wa juhudi za kutafuta muarobaini wa kudumu wa huduma za afya kwa wote, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya uongozi wa Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeanzisha jumla ya madirisha 1,066 ya kutolea huduma za afya kwa wazee, kwenye hospitali 187 na vituo vya afya 879 katika halmashauri 184.

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, alielekeza utambuzi wa watoto walio katika mazingira hatarishi, ambapo watoto 284,308, kati yao 183,124 wakiume na 101,184 wakike, walitambuliwa na kupatiwa huduma zikiwemo mafunzo ya ufundi stadi, kadi za bima ya afya ya Jamii, vifaa vya shule na kuwaunganisha na familia zao.

Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, imesimamia uundwaji wa kamati za watu wenye ulemavu 7,518, kamati za ulinzi na usalama wa mwanamke na mtoto 18,126 pamoja na mabaraza ya ushauri ya wazee 20,748 katika ngazi mbalimbali za mikoa, halmashauri, kata, vijiji na mitaa, kote nchini.

Tayari Serikali ya Rais Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeshasimamia ushughulikiwaji wa mashauri takriban 2,682 ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, migogoro ya ndoa na familia 5,306.

Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amejitoa kuhakikisha huduma mbalimbali zikiwemo, misaada ya kisaikolojia na kijamii, huduma za afya, matunzo kwa watoto, malazi, huduma kwenye za msingi kwenye vituo jumuishi, mavazi, chakula, kuwaunganisha manusura wa vitendo vya ukatili na familia zao pamoja na kutoa rufaa kwenda kwenye huduma mbalimbali iliwemo mahakamani, zinatolewa kikamilifu ili kuponya kundi kubwa lililokuwa limesahaulika na jamii.