728 x 90

Chama kuiongezea nguvu Yanga kimataifa.

  • July 1, 2024
Chama kuiongezea nguvu Yanga kimataifa.

Usajili wa kiungo wa kimataifa wa Zambia, Clatous Chota Chama, uliotangazwa na Yanga, unatazamiwa kuiongezea nguvu Klabu hiyo kwenye michuano ya kimataifa ya klabu bingwa ya Afrika.

Chama aliyemaliza mkataba na mahasimu wa Yanga, Simba, anjiunga na kikosi cha Yanga ambacho kilionyesha ubora mkubwa kwenye mashindano ya klabu bingwa barani Afrika msimu uliopita.

Kwa ubora alionao Chama na uzoefu wa mashindano makubwa ni wazi kutaongeza ushindani wa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Yanga ambacho tayari kimesheheni nyota kadhaa wenye uwezo mkubwa kama Aziz Ki, Max Nzengeli, Pacome, Mudathir Yahya na wengine wa nafas za viungo washambuliaji.

Mwalimu wa Yanga Miguel Gamondi ambae nae aliongeza mkataba wa kuitumikia Yanga, anapata nafasi nyingine ya kurudi kwenye mashindano makubwa akiwa na silaha nyingine kubwa ambayo imeshacheza mashindano mengi ya kimataifa.