728 x 90

Tafsiri ya Mchungaji Msigwa kuhamia CCM

  • July 1, 2024
Tafsiri ya Mchungaji Msigwa kuhamia CCM

Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA ametangazwa kuhamia Chama Cha Mapinduzi baada ya miaka mingi ya kuhudumu kama nguzo muhimu ya kambi ya upinzani.

Kuhamia kwake Chama Cha Mapinduzi kunatafsiriwa kama pigo kuu kwa chama kilichotarajiwa kuchuana vikali na Chama Cha Mapinduzi katika chaguzi zjiazo za Serikali za Mitaa na baadae mwakani, Uchaguzi Mkuu.

Ni dhahiri bila shaka kuwa Mchungaji Msigwa amevutiwa na aina ya utendaji wa Rais wa awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambae amekuwa chachu ya mageuzi ya kimkakati, hasa ya kiuchumi, yanayoendelea kuibadili taswira ya Tanzania.

Msukumo mkubwa wa Mchungaji Msigwa unatajwa kuwa, kukimbilia mahali demokrasia inapotawala tofauti na mazingira ya hujuma yaliyojitokeza katika uchaguzi wa kanda wa CHADEMA.

Azma ya Mchungaji Msigwa ni kushiriki kikamilifu katika mageuzi makubwa ya kiuchumi kwa kuwa na mchango wa moja kwa moja wa mawazo na hoja katika ilani ya uchaguzi na ushiriki wa utekelezaji wake.

Haiba ya sasa ya ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, inatajwa pia kuwa sehemu kubwa ya kumshawishi Mchungaji Msigwa kuamua kujiunga na Chama Cha Mapinduzi.

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa muumini wa utawala bora, unaozingatia sheria, uwezeshaji wa kiuchumi, uboreshaji wa huduma za kijamii kama afya, elimu, maji na ustawi wa jamii kiujumla.

Kitendo cha Chama Cha Mapinduzi kumpokea na kumtambulisha Mchungaji Msigwa, wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa, kinatoa ishara ya ukomavu wa chama chenyewe na utayari wa kuweka kando tofauti za nyuma kwa manufaa ya kulijenga Taifa.

Ushawishi wa kujenga hoja alionao Mchungaji Msigwa, na kuwasilisha mada, pamoja na utashi wake wa kusimamia miradi utakiongezea Chama Cha Mapinduzi hazina kubwa ya viongozi wenye haiba ya kubeba majukumu makubwa ya kitaifa.

Ujio huu wa Mchungaji Msigwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi ni ushindi na ushahidi mwingine wa uwezo wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuliongoza Taifa. Tafsiri ya taarifa ya kuhama kwa Mchungaji Msigwa ni kuwa, hata vyama vya upinzani nchini, vinavutiwa na uchapakazi, weledi na uzalendo wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.