728 x 90

Serikali yakusudia kuanzisha tozo ya maendeleo ya viwanda kulinda viwanda vya ndani.

  • June 27, 2024
Serikali yakusudia kuanzisha tozo ya maendeleo ya viwanda kulinda viwanda vya ndani.

Serikali kupitia mapendekezo ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 inakusudia kuanzisha Tozo ya Maendeleo ya Viwanda kwa baadhi ya bidhaa zinzoingizwa nchini.

Hatua hii itatumika kama mbinu ya ziada ya kuvilinda viwanda vya ndani dhidi ya ushindani usio sawa wa bidhaa zinazotoka nje na kwa jinsi hiyo kuchochea mauzo ya nje ya nchi.

Serikali imetoa mapendekezo ya kusaidia kuendeleza sekta ya viwanda nchini hasa vile viwanda vidogo na vya kati kupitia fedha zitokanazo na tozo hiyo.