Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imependekeza kuweka tozo ya asilimia 10 kwenye mafuta ghafi ya kula ya alizeti na mashudu yanayotokana na mbegu za alizeti pamoja na mbegu za alizeti zinazosafirishwa kwenda nje ya Jamhuri ya Muungano.
Lengo la mapendekezo haya ni kuhakikisha malighafi hizo zinapatikana kwa wingi nchini ili kuzalisha mafuta ya kula, kuondoa changamoto ya uhaba wa mafuta pamoja na chakula cha wanyama.